BANK
Article Pic

A Tasty – Secure Password Recipe

Kamati ya kuweka passwords kama 1234…kujeni mbele ya class. Mfuatwe na ile kamati ingine yenye inatumia the same password kila mahali. Na kabla sijasahau the special one’s wale wa kuweka jina yao kama password, please join wenzenu mbele ya class.

Ushai hackiwa ikae kama rumuors?- Password basics kama hizi zitakucost vibaya sana.

Lakini relax—sina lecture. Kaa chini niwafunze kupika mazigizaga.

First things first, creating a strong password ni kama kupika favorite dish yako. Secondly, tukubaliane tu sahii mambo ya kureuse passwords ama kuweka birthday yako – tuwache.

Now, let’s cook this thing up right!

Ingredients tunatumia:

Letters, Numbers, Special Characters na attention kiasi🧠

Instructions

  1. Mix up password yako na small letters, capital letters, numbers and special characters (*^@) Na kama tu spices za biryani, the longer the password, the stronger it is!
  1. Kwa wenye memory ni kichungi, tumia passphrase iko easy kukumbuka. E.g. ChaiTamu@7Asubuhi. Wanja, kamum usicopy hii aki. Of Importance ni ukicreate password usiende kuambiana ama kuandika sticky note. Hiyo ni kama kusema “karibuni hackers, the door is open!” 🚪
  1. Lastly, tia garnish ama mazigizaga na Multifactor Authentication (MFA). MFA ni kama ile garnish ya mboga ya kienyeji—haiwezi kosa kwa recipe serious. MFA inakuongezea layer ya security juu hakuna msee anaweza access account yako bila permission yako!

What do I mean?

MFA itakuitisha permission on email or SMS for every login attempt ndio ujue kama rada yako ni chafu.

Vitu rahisi na very necessary.

Si recipe ya kuwa safe ni simple? Kaa chonjooo!

 

Over and out,

Witty Banker

Nov 05, 2024 Trending

Popular Articles